JINSI YA KUTENGENEZA OKRA WATER
🥒 Jinsi ya Kutengeneza Okra Water
Vitu unavyohitaji:
Kikombe 1 cha maji safi
Namna ya kutengeneza:
1. Osha bamia vizuri na kata ncha zake.
2. Kisha zikate vipande vidogo.
3. Weka vipande hivyo ndani ya kikombe cha maji safi.
4. Funika na uache usiku kucha (masaa 8–12).
5. Asubuhi, toa vipande vya bamia na kunywa maji yake ukiwa tumbo tupu.
🌿 Faida za Okra Water
✅ Husaidia kupunguza uzito – inasaidia kutuliza njaa na kuboresha mmeng’enyo wa chakula.
✅ Nzuri kwa ngozi – vitamini C na antioxidants zake husaidia kuondoa uchafu mwilini na kutoa glow ya asili.
✅ Hupunguza sukari mwilini – wagonjwa wa kisukari hutumia mara nyingi kusaidia kushusha kiwango cha sukari.
✅ Huboresha afya ya moyo – husaidia kupunguza cholesterol mbaya (LDL).
✅ Huimarisha nywele – maji yake yanapokunywa mara kwa mara, husaidia nywele kukua na kuwa na afya.
✅ Huongeza nguvu mwilini – hutoa madini na vitamini vinavyoongeza stamina na kinga ya mwili.
📌 Vidokezo vya Kutumia
Kunywa kikombe kimoja tu asubuhi.
Usizidishe kwa sababu ni tiba asilia (mara 3–4 kwa wiki inatosha).
Wajawazito au wenye matatizo ya kiafya watalazimika kushauriana na daktari kwanza.
#AggieGlowTips #OkraWater #AfyaNaUrembo #AsiliNiTiba #HealthyLiving #majiyabamia
.png)
.jpg)
Comments
Post a Comment